Saratani ya shingo ya kizazi

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi.Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.

Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani ya nne inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50 ,000.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika waliopata fursa ya utafiti.

NINI KISABABISHACHO SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ?
Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana.


BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo au chini ya miaka 18Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofautiUtumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama UkimwiUzazi wa mara kwa mara



Dalili za ugonjwa saratani ya shingo ya kizazi
1. Kutokwa na damu ukeni kusiko kawaida mfululizo
2. Kupata maumivu makali ya tumbo na nyonga
3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
4. Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida.
5. Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia
6. Mkojo wenye matone ya damu.

Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
Mgonjwa anapofika kituo cha afya hufanyiwa kipimo cha Pap test. Kipimo hichi kinajumuisha kuchukuliwa kwa sample ndogo ya seli zilizoathirika kwenye cervix ili kugundua kama kuna mabadiliko na uwepo wa seli za saratani.
Watu gani wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya shingo ya kizazi zaidi:
Kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo unaweza kuzifanyia kazi na kuunguza hatari ya kupata saratani hii, japo pia kuna njia ambazo ni vigumu kuepuka za ziko nje ya uwezo wetu kama vile uwepo wa saratani hii katika historia ya familia yako mfano kama mama ama dada yako aliwahi kupata saratani hii basi unaweza kuwa kwnye hatari kubwa nawe kupata. Makundi mengine ni kama
Wanawake kwenye umri kati ya miaka 20-50 wapo kwenye hatari Zaidi
Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongzeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi.
Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata saratani hii.

JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA ?

Matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi
Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, na inahusisha
Kufanyiwa upasuaji na kuondoa mfuko wa mimba (uterus) na viungo vingine kama ovari na mirija ya uzazi
Matibabu kwa kutumia dawa kali(chemotherapy) ili kuongeza muda wa kuishi
Matibabu kwa njia ya mionzi ili kuua seli za saratani.

Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.

PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);Pap-Smear ni test ambayo hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.
UMRI WA KUPATA PAP TESTTest hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya umri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa kwa kipindi cha kisichopungua miaka 3.
USHAURI WABKITABIBU
             KUPUNGUZA HATARI ZA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI
Pap tests.  Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.
Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari)
Kuwa na mpenzi mmoja. Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.
Tumia kinga (condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa mengi ya zinaa

About Dr.Mkojera

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

Dealing with health related issues

Forex

//graizoah.com/afu.php?zoneid=3455041