LISHE YA MTOTO WA MIEZI 6-9

Lishe bora kwa mtoto wa miezi sita mpaka tisa.


Wataalamu wa afya wanashauri kuhusu umhuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto wa siku moja mpaka miezi sita bila kumpa kitu kingine,ikiwa ni maziwa ya kopo,ya ng’ombe au uji hii ni kwa faida ya afya ya mama na mtoto pia. Kunyonyesha ndo njia nzuri na ya kwanza kumpa mtoto chakula. Mtoto anayepewa maziwa ya mama kwa uhakika ndani ya miezi sita ya mwanzo afya yake ni ya tofauti sana na mtoto ambaye amenyimwa maziwa hayo,au amepewa kwa kiwango kidogo.
Na faida haipo kwa mtoto tu ila mama pia inamsaidia,

1. kumpa kua karibu na mtoto wake na kumuelewa.

2. Hupunguza uwezekano wakupata kansa ya matiti.
3. Zaidi huondoa gharama zisizo na ulazima kwani maziwa haya yanatoka kwako,na inamuepushia mtoto kua na uwezekano wakupata allergies,ambazo zinaweza kuchukua muda wako na pesa yako kutibu.
Wakati ambao unaweza kumpa mtoto vyakula vingine.

Unaweza kumpa mtoto vyakula vingine kwanzia miezi minne hii pia inatokana na ushauri wa kidaktari ila kama inawezekana subiri mpaka miezi sita,na unapoanza kumjaribishia mtoto vyakula vingine haimaanishi kua utatakiwa kumuachisha kunyonya. Hapana utampa vyakula na utamnyonyesha mpaka umri wa miaka miwili na nusu ili kumsaidia mtoto kua na afya njema.
Unaweza kuangalia mambo kadhaa kugundua kama mtoto yupo tayari kupata vyakula vingine.
Awe na miezi sita kwenda mbele,kumbuka pia kuangalia ushauri wa kidaktari.
Unapompa chakula anakua anakipokea mdomoni tayari kukimeng’enya na si anatema nje.
Hakikisha shingo yake imeshaanza kukaza.
Mwanzishe mtoto wako na lishe hii.
Ukiendelea kumnyonyesha mtoto wako. Anza kumpa vyakula vyenye madini ya chuma ni muhimu kwake,pia jaribu kumpangia ratiba inayoeleweka na itakayofuatwa na mara nyingine weka ratiba ya kula naye pamoja kama familia,kama kuna watoto wenzake hapo nyumbani mlishe wakiwa nao wanakula karibu yake ili kumpa hamasa ya kutamani chakula.
Hakikisha vyakula vyake vinakua vimepondwa pondwa kabisa,viwe vilaini kumbuka koo lake bado dogo. ikiwezekana tumia blender kabisa.
Hakikisha kwenye mlo wake kunakua na mlo kamili yani matunda na mboga mboga,mbegu,nafaka,nyama na samaki.
Usimchanganyie mtoto wa miezi hii nafaka mbali mbali kwenye uji wake,inashauriwa kumpa aina moja ya uji,unaweza kumuwekea ratiba kama ni uji wa sembe mpe sembe tu,kama ni ulezi au mchele muekee ratiba ila usimchanganyie.
Usimpe mtoto chakula kilichobaki jana yake,mtengenezee mlo wakumtosha siku hiyo,epuka kumpashia vyakula vilivyolala na hakikisha vyakula vyake vunatengenezwa kwa usafi wa hali ya juu.
Matunda kama papai,parachichi na maembe ni mazuri kwakuanzia. unaweza chemsha njegere,maharage au mboga za majani na kumpa supu yake kidogo,weka chumvi kidogo sana,isisikike kabisa kwenye mlo wake.
Usimpe vyakula vya madukani kwa miezi hii,kama ni juice tengeneza mwenyewe kwenye hali ya usafi na usmchanganie matunda kwa wakati mmoja,pia jaribu usimpe mlo mmoja mda mrefu mpaka kukinai chakula hicho.

Usafi wakati wa uandaaji wa chakula cha mtoto ni muhimu.

1. Mikono yako iwe misafi wakati unaanza kuandaa vyakula.
2. Vyombo utakavyo tumia viwe safi na salama.
3. Matunda na vyakula vyote vihifadhiwe kwenye hali ya usafi.
4. Vyombo vya mtoto vitenge visitumike au kuchanganyika na vyombo vingine vya nyumbani.
5. Atakayekua anamhudumia mtoto kwenye chakula uhakikishe ni mwenye hali ya usafi na ukanye kusiwe na kulamba chakula cha mtoto kwenye chombo chake kwa madai ya kupooza na kumlisha mtoto,kwani ni hatari kwa afya yake.
Kumbuka afya bora ya mwanao ni furaha yake na furaha kwako pia,utakapomwangalia na kujali afya yake utampa nafasi yakutabasamu na kua mwenyenguvu na kukupa kua mama bora kwa watu wanaokuzunguka na jamii itaiga mfano wako. Linda afya ya mwanao kwa lishe bora.

About Dr.Mkojera

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

Dealing with health related issues

Forex

//graizoah.com/afu.php?zoneid=3455041