Homa ya ini (hepatitis) ni neno linalotumika kujumuisha magonjwa yote yaletayo madhara kwenye ini, hushambulia na kudhuru seli za ini. ugonjwa huu unaleta madhara makubwa kwenye ini ikiwa ni pamoja na kuacha makovu, japo kua pia wa weza kupona bila kusababisha madhara kwenye ini la binadamu. Homa ya ini huweza kudumu hata kwa muda upatao miezi sita, au zaidi ya miezi sita
Kuna aina takribani tano za ugonjwa huu wa homa ya ini. Aina hiza za homa ya ini zote zinasababishwa na virusi vya homa ya ini. Tafiti zinaonesha kua takribani watu milioni 250 duniani wanasumbuliwa na hepatitis C. Watu wapatao milioni 300 wanashambuliwa na wanaweza wanaweza kueneza hepatitis B
Aina nyingine za ugonjwa huu kama hepatitis A,D na E pia hushambulia seli za ini sambamba na hilo virusi ambavyo hushambulia na kusababisha uharibifu mkubwa wa seli za ini ni hepatitis A,B na C. Pia kuna ugonjwa wa homa ya ini usio sababishwa na virusi nao ni hepatitis X.
Hepatitis G Virus (HGV) hutokana na kirusi cha pekee kabisa. Pia zipo aina nyingine za hepapitis amabazo haziambukizwi, unywaji wa pombe matumizi ya dawa zenye kemikali pia huweza kusababisha uharibifu wa maini.
Pia madhara ya homa ya ini huweza kurithiwa. Iwapo mtu atazaliwa kwenye familia yenye historia ya ugonjwa huu. Upungufu wa kinga mwilini hupelekea ugonjwa huu pia ulafi huweza kuwa chanzo cha tatizo hili.
kipindi kinachofuata tutaelezea kwa kina dalili za ugonjwa huu wa homa ya ini.