MAZOEZI NA UMUHIMU WAKE KWA WAJAWAZITO

Mama mjawazito anashauriwa afanye mazoezi mepesi mepasi karibuni kila siku katika kipindi chake chote cha ujauzito. Ikilinganishwa na miongo kadhaa hapo nyuma, nyakati hizi wajazito wengi wamekua wakishauriwa na wataalamu wa afya kujihusisha na swala zima la ufanyaji wa mazoezi. mazoezi huimarisha afya ya mama pamoja na mtoto.


Miongo kadhaa iliyo pita lilikua ni jambo la kawaida kusikia jamii yetu ikimshauri mama majamzito kupumzika kadri awezavyo wakidhani kuwa mazoezi yanaweza pengine kusababisha uchungu wa ghafla ama kuharibu kabisa kiumbe aliyepo tumboni
 Ni vema mama mjamzito kufanya mazoezi ya mwili na kuweka misuli sawa wakati wa ujauzito wake na hata baada ya kujifungua kwani hii humjengea afya bora ikiwa ni sambamba na kula mlo kamili. Kupitia mazoezi haya afya ya mama na mtoto aliyeko tumboni huimarika mara dufu.

je mazoezi haya yafanyike kwa muda gani?
Wataalamu hushauri mazoezi madhubuti yafanyike kwa muda kati ya dakika 10 mpaka 30 mimba isiwe na matatizo mengineyo yoyote yale. pia mazoezi haya madhubuti kabisa ni muhimu sana kwa wajawazito ambao shughuli zao za kila siku sio za kutosheleza kuifanya miili yao kua tahshishi.

Mazoezi yapo ya aina nyingi sana ambayo mtu wa aina yeyote ile anaweza kuyafanya na yakamsaidia kulinda na kujenga afya imara, mazoezi haya hayafungaman na umbile ama umri wa mtu yeyote yule.
Mama mjamzito anaweza kufanya mazoezi ya kutembea au kukimbia taratibu, lakini pia kama ni mpenzi wa kuogelea pia ni moja ya mazoezi mazuri yanayopendekezwa na wataalamu weng wa maswala ya wanawake. Wengi hupenda aina hii ya mazoezi kwani ni rahisi mno kwa kunyoosha viungo vya mwili.


faida za mazoezi wakati wa ujauzito.



      1. Husaidia kujenga na kuimarisha afya ya mama na mtoto
      2. Kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
        • kisukari cha ujauzito
        • shinikizo la damu
        • pia husaidia uwezekano wa kupasuliwa wakati wa kujifungua.



Wakati wa mazoezi ni vema ukawa makini na aina ya zoezi unalolifanya kusudi lisije likawa na madhara kwako na kwa mtoto, jiepushe na michezo ya kugusana kama mpira na mingine yote yenye jamii hyo pia vaa viatu vyenye kisigino kifupi wakati wa mazoezi pia visiwe na soli itakayokupelekea uteleze kwa urahisi, epuka michezo ya kuzama majini wakati wa ujauzito kwani ni hatari sana. pia kupanda milima mirefu ni hatari kwa afya yako na mtoto.

About Dr.Mkojera

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

Dealing with health related issues

Forex

//graizoah.com/afu.php?zoneid=3455041